HEKIMA (SWAHILI/CONGO)
SALA YA SOLOMONO YA KUMWOMBA MUNGU HEKIMA
IMETOLEWA KWA KITABU CHA HEKIMA 9:1-18
Omba hii sala mara mingi kila siku. Ipatie watu wengi pia waombe Mungu wapate hekima. Sala zingine zapatikana kwa website hii: www.avemaria832.simplesite.com Tangaza hii kwa watu wote ukitumia facebook etc.
- Mungu wa mababu na Bwana wa huruma, uliyeumba ulimwengu kwa neno lako,
- na kumtunga mwanadamu kwa hekima yako, ili avitawale viumbe vilivyo anzishwa na wewe, auongoze ulimwengu kwa utakatifu na haki,
- atawale kwa unyofu wa moyo;
- Unipe hekima iketiyo kitini mwako, usinitenge mbali na watoto wako.
- Kwa maana mimi ndimi mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako, mtu mzaifu mwenye maisha mafupi, mjinga kwa habari za haki na sheria.
- Kama mtu fulani angekuwa mtimilifu kati ya wanadamu, lakini angekosa hekima itokayo kwako, huyu angestahili kuhesabiwa kama si kitu.
- Ulinichagua mimi niwe mfalme wa taifa lako, mwamuzi wa waana wa kiume wako na mabinti yako.
- Ukaniagiza nijenge hekalu juu ya mlima wako mtakatifu, na altare mjini unamokaa, kwa mfano wa hema takatifu uliyo weka tayari tangu mwanzo.
- Kwako iko hekima ijuayo kazi yako iliyokuwapo ulipoumba ulimwengu. Nayo hujua yapendezayo macho yako, yaliyo maadilifu kadiri ya amri zako.
- Uitume kutoka kiti chako kitukufu iwe msaidizi katika shuruli zangu, nitambue yakupendezayo.
- Kwa maana hekima yajua yote na kuyafahamu, nayo itaniongoza kwa utaratibu katika vitendo vyangu; itanikinga kwa nuru yake nyangavu.
- Ndipo hapo kazi zangu zitapendeza, nitalitawala taifa lako kwa usawa, nitakuwa nimekistahili kiti cha baba yangu.
- Ni nani awezaye kujua nia zake Mungu? Ni nani awezaye kuwaza mapenzi yake Bwana?
- Kwani mawazo ya wanadamu yanasita, na fikara zetu zinabadilika.
- Kwa maana mwili utakao oza huitia roho uzito, na hema hiyo ya udongo huelemeza akili yenye shuruli nyingi.
- Kwa shida tuyafahamu yaliyo duniani, na kwa ugumu tuyapata yaliyo mikononi mwetu; lakini ni nani aliyevumbua yaliyo mbinguni?
- Ni nani aliyepata kujua nia zako, isipokuwa Wewe umetoa hekima, na kutuma roho yako takatifu kutoka juu?
- Ndivyo zilivyonyoshwa njia zao walio duniani, ndivyo wanadamu walivyofundishwa yanayokupendeza, na kuokolewa na Hekima.