HEKIMA (SWAHILI/KENYA)
SALA YA SOLOMONI YA KUMUOMBA MUNGU HEKIMA
INAOMBWA KUSOMA KILA SIKU NA WAKRISTU
IMETOLEWA KWA KITABU CHA HEKIMA 9:1-18
Omba hii sala mara nyingi kila siku. Ipatie watu wengi pia waombe Mungu wapate hekima. Sala zingine zapatikana kwa website hii: www.avemaria832.simplesite.com Tangaza hii kwa watu wote ukitumia facebook etc.
- Ee Mungu wa babu, na Bwana wa rehema, ambaye ulivifanya vitu vyote kwa neno lako
- Na kwa Hekima wako ulimwumba mwanadamu apate kuvitawala viumbe vilivyofanywa nawe,
- Na kuuongoza ulimwengu kwa utakatifu na haki, na kutoa hukumu kwa unyofu wa moyo;
- Unipe Hekima, anayeketi karibu na kiti chako cha enzi, wala usinikatae miongoni mwa wana wako,
- Kwani mimi ni mtumishi wako na mwana wa mjakazi wako; mtu dhaifu, na muda mfupi wala sina nguvu za kuzielewa hukumu na sheria.
- Maana, hata kama mtu angekuwa mkamilifu kuliko wanadamu wote, mbali na Hekima atokaye kwako, angehesabiwa si kitu.
- Wewe ulinichagua kuwa mfalme wa watu wako na mwamuzi wa wanao na bintizo.
- Uliniamuru kujenga hekalu katika mlima wako mtakatifu, na altare katika mji wa makao yako, mfano wa hema takatifu uliyoitengeneza tayari tangu mwanzo.
- Na Hekima yu pamoja nawe, naye hujua matendo yako alikuwa karibu ulipofanya ulimwengu; anafahamu ni nini kinachopendeza machoni pako, na nini ni sawa kadiri ya amri zako.
- Mpeleke kutoka mbingu takatifu, na kumtuma kutoka kiti chako cha enzi cha utukufu, Apate kutaabikia kazi pamoja nami, nami nijue ni nini kinachokupendeza.
- Maana Hekima hujua na kuelewa mambo yote, naye ataniongoza kuwa na kiasi katika kutenda kwangu, naye atanilinda katika utukufu wake;
- Na hapo, matendo yangu yatakupendeza, nami nitawahukumu watu wako kwa haki, na kustahili kiti cha enzi cha baba yangu.
- Maana nani kati ya wanadamu aweza kujua mashauri ya Mungu? Au kutafakari atakayo BWANA?
- Kwani mawazo ya wenye kufa yana uoga, na fikra zetu zina hatari.
- Maana mwili uharibikao huilemea roho na hema ya udongo hukandamiza akili yenye kujaa mawazo.
- Ni vigumu kwetu kuyapambanua mambo ya duniani, na ni kazi ngumu kuyaona yaliyo mikononi mwetu; basi, yale yaliyo mbinguni nani atayachunguza?
- Nani aliweza kuyajua mashauri yako, isipokuwa wewe ulimpa Hekima, na kumpelekea roho yako takatifu kutoka juu?
- Ndivyo yalivyonyoshwa mapito ya walio juu ya nchi nao wanadamu walifundishwa mambo yanayokupendeza, na wakaokolewa na Hekima.